Kuhusu Mwalimu Hemedi
Personal life
Jina langu ni Abdallah Hemedi, but the name with title ni Mwalimu Hemedi. Ni Baba, Mwalimu, Mwandishi na Mjasiriamali. Ninaishi with my beautiful wives S and A na Watoto Wetu.
Familia ni moja ya furaha yangu kubwa ya maisha na ni zawadi yenye thamani kubwa mno kwangu, Mara nyingi natumia baadhi ya nyakati katika siku kukaa na familia na kufurahia maisha kwa pamoja.
Napendelea kujifunza vitu vipya kila siku na kuwashirikisha watu wengine maarifa ninayopata.
Napendelea kusoma vitabu na makala mbalimbali mtandaoni hasahasa kuhusu branding na marketing.
Professional life
Kiu yangu kubwa ya kufahamu kompyuta na internet ilianza mwaka 2008 ambapo Kampuni ya Vodacom ilikuja kuzindua mnara katika kijiji chetu kilichopo mkoani Lindi.
Walileta vipeperushi vyenye kueleza huduma zao, simu wanazouza na huduma ya internet, nilivutiwa sana kusoma vipeperushi hivyo na nilishikwa na hamasa ya kufahamu kuhusu internet lakini wakati huo sikuwa na simu.
Mwaka 2009 kuna Waitaliano walitembelea kijijini kwetu na mimi nikapata bahati ya kuwa mkalimani msaidizi kwani walikuwa wanajua na kiingereza pia.
Waitaliano hao walikuja na kompyuta na walikuwa wanatumia internet, hapo kiu yangu ya kujua internet iliongezeka lakini sikupata nafasi ya kutumia kompyuta zao kwani zilikuwa ni binafsi kwao.
Mwaka 2012 mwishoni nilifanikiwa kupata simu yenye uwezo wa internet, hapo nilianza kujifunza kuhusu internet lakini kutokana na simu kuwa na uwezo mdogo sikuweza kufanya vitu vingi.
Mwaka 2013 niliweza kutengeneza blog yangu ya kwanza kabisa (kwa sasa haipo nilishaifuta).
Mwaka 2014 niliifahamu platform ya WordPress ambayo inatumika kutengeneza blog na websites lakini kwa kipindi hicho niliweza kutengeneza blogs tu.
Mwaka 2014 pia nilifahamiana na Amani Makirita (Mtanzania) na nikaanza kufatilia makala zake kuhusu biashara na ujasiriamali pia mwaka huohuo 2014 nikamfahamu Syed Balkhi (Mmarekani) ambaye amejikita kutoa mafunzo mbalimbali ya wordpress na kutengeneza kipato kupitia mtandao wa internet.
Pia nikamfahamu Lalit Kumar (Muhindi) ambaye anafundisha mbinu mbalimbali za kutengeneza kipato kupitia internet.
Kuanzia mwaka 2012 nilipoanza kutumia internet hadi mwaka 2015 sikuwahi kuingiza pesa yoyote kupitia internet, ila sikukata tamaa niliendelea kujifunza kwa nguvu zote.
Mwaka 2015, 2016 niliendelea kujifunza mambo mbalimbali mtandaoni, na katikati ya mwaka 2016 nilianza kutengeneza kipato kwa kuwatengenezea blog watu mbalimbali.
Ilikuwa ni furaha kwangu kwani nipo nyumbani tu kijijini lakini nawasiliana na watu mbalimbali na wananiamini nafanya kazi zao na wananilipa kwa AirtelMoney.
Nikiwa chuoni (2016, 2017, 2018, 2019) Niliendelea kujifunza na kuwashirikisha maarifa niliyonayo watu wengine kwa njia mbalimbali na ilipofika mwezi Aprili 2019 niliandaa mafunzo ya Microsoft Excel for Teachers kwa mfumo wa Video na baada ya watu kujifunza kozi hiyo walishauri niandae kozi zaidi za program nyingine za kompyuta.
NB: Ujuzi wa kompyuta na mtandao nimesomea online tu, na sababu hiyo ndiyo imenipa hamasa pia ya kuandaa mafunzo kwa mfumo wa videos ili yawasaidie hata watu waliopo mbali na mimi au wasiokuwa na muda wa kufika chuoni kusoma.
Kwenye ujuzi wa Kompyuta na Biashara nimejifunza Vitu Vingi sana kutoka kwa wafuatao (Ninathamini mchango wao Kwangu)
- Mr. Makirita Amani (Kutoka Tanzania) – Nimejifunza Ujasiriamali na Blogging
- Mr. Syed Bakhi (Kutoka Marekani) – Nimejifunza WordPress na Online Business
- Mr. Lalit kumar ( Kutoka india) –Nimejifunza Blogging na Online Passive Income
- Dr. Said Said ( Kutoka Tanzania (Zanzibar)) – Nimejifunza WordPress na Ujasiriamali.
- Madam Leila Gharani (Kutoka Austria) – Nimejifunza Excel
- Mr. Jon Morrow ( Kutoka Marekani) –Nimejifunza uandishi, blogging na Uthubutu.
- Brian Tracy (Kutoka Marekani) – Nimejifunza Uandishi, Marketing, Uthubutu.
- Mr. Pavan Lalwan (Kutoka India) – Nimejifunza Excel
- Mr. Adam Preiser ( Kutoka Marekani) – Nimejifunza wordpress.
- Mr. Arek Dvornechuck (kutoka Marekeni) – Nimejifunza Branding
- Madam Lindsay Marsh ( Kutoka Marekani) – Nimejifunza Adobe Photoshop, Illustrator & InDesign.
- Mr. Sabri Suby (Kutoka Australia) – Nimejifunza Digital Marketing
Ahsante kwa kusoma! Ungependa kusoma makala zangu? Bonyeza hapa
