Nitakuandalia Logo Nzuri na Inayoendana na Biashara Yako
Logo ni nembo au alama inayotambulisha biashara yako na kushikilia thamani ya brand (chapa) yako kibiashara. Logo ni kitu muhimu sana katika biashara yako.
Umuhimu wa Logo katika Biashara Yako.
1. Logo inatambulisha biashara yako: Watu wanaitambua biashara yako kwa urahisi ikiwa unatumia logo sahihi na inayoeleweka. Hivyo kukosa logo inapelekea watu kutoitambua biashara yako kwa urahisi.
2. Logo inaifanya biashara yako kuwa ya kipekee: Logo ya biashara yako inakutofautisha na biashara nyingine zilizopo na hivyo inaipa upekee biashara yako.
3. Logo inajenga uaminifu kwa wateja: Mteja akishapata huduma kwako na akaiona logo ya biashara yako na akaitambua na iwapo bidhaa zako ni nzuri hivyo mteja atakuwa anaamini bidhaa zenye logo yako.
4. Logo inaongeza ufanisi katika kutangaza biashara yako: Ukiwa na logo inasaidia sana katika kutangaza biashara yako, watu wataiona na kuitambua biashara yako kwa urahisi zaidi tofauti na biashara ambayo haina logo inakuwa ni vigumu kutambulika kwa urahisi.
BAADHI YA LOGO NILIZOTENGENEZA






Je, Ungependa Nikuandalie Logo ya Biashara Yako?
Jaza fomu hii kuagiza Logo yako, Logo yako itakamilika ndani ya siku 2 hadi 3.
Gharama ya Logo ni Tsh 40,000 TU Utapatiwa Picha ya Logo na Mockups pamoja na Brand Colors
